Monday, November 28, 2011

Siku hizi ni kwa vichanga!



Bado tunaendeleza mila. Kuna jamii (kabila) zaidi ya 16 mkoani Mara zinazojihusisha na ukeketaji kwa watoto wa kike. Msimu ndo huu baada ya mavuno, mbali na wasichana ambao hawako tayari kutukanwa na wenzao visimani kuwa ni 'wasagane', sasa hali imehamia kwa vichanga, majumbani ama kwa kushirikiana na manesi huko mahospitalini.

Ile sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) imelala fofofo!

Friday, November 25, 2011

Mifumo yetu ya kuzuia majanga i wapi?

Leo usiku na asubuhi baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma wamejikuta wakiwa hawana nyumba ama nyumba zao kuzingirwa na maji kimo cha magoti ya mtu mzima!

Na wala si makazi ya watu tu bali zahanati ya serikali ya Bweri na pia ile inayomilikiwa na kanisa la AIC zimejikuta zikiwa zimezingirwa na maji kotekote!

Mpaka sasa hakuna madhara ya upotevu wa maisha uloripotiwa kutokea lakini adha hii ingeweza kuepukika.

Binafsi naona uchovu wa wataalamu wetu wa kuzuia majanga na pia wataalam wa mipango miji.

Maana mahali ambapo bonde na hapakustahili kuwa makazi ya watu hawa waheshimiwa wamepima viwanja vya makazi ya watu.

Kazzi kweli kweli.

Sunday, November 6, 2011