Monday, October 31, 2011

Kaazi Kweli Kweli!


Yawezekana mambo yako hivo nchi nzima?

Sunday, October 30, 2011

Dunia Ina Mambo!

Sina la kusema zaidi ya kusikiza muziki huu! Muwe na Jumapili njema!

Saturday, October 29, 2011

Sijui kama tuna Wasimamiaji wa Maamuzi!



Tarehe 20 Oktoba nilisafiri na basi la Akamba tokea Arusha lenye nambari za usajili KBJ334J lililokuwa linatoka Dar kwenda Nairobi.

Nilifurahi jinsi lilivyokuwa likipita chap chap mpakani.... Kufika katika viunga vya jiji la Nairobi vikaanza kushushwa viroba vya SUKARI kilo 25 toka kiwanda cha Kilombero.

Nikajiuliza...watu wa forodha na wengineo hawapo mpakani? Maagizo ya kutovusha sukari hawayasikii?


Akili kwako.....

Friday, October 28, 2011

Kumbe kuna Al Shaabab hapa nchini?

Ati maandamano yasitishwa kwa sababu ya Al Shaabab!


Kama ndivo basi nadhani sherehe za kuzima mwenge wa uhuru zilizopangwa kufanywa tarehe 1 Desemba na pia sherehe za Uhuru 9 Desemba hazitakuwepo!!!


Mmmmmh!

Hatimaye Afanyiwa Upasuaji

Hatimaye Kaka Shaban Kaluse amefanyiwa upasuaji kufuatia ajali ya gari iliotokea juzi asubuhi. Upasuaji ulifanyika saa 6 usiku wa kuamkia leo.

Amelazwa wodini na anaendelea vema japo mkono ulivimba sana mara baada ya upasuaji.

twamuombea apone haraka.

Wednesday, October 26, 2011

Maandamano kupinga ulipwaji wa Dowans



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
MAANDAMANO YA KUPINGA SERIKALI KUILIPA DOWANS Sh. BILIONI 111
Novemba, 2010 Mahakama ya usuluhishi ya kimataifa ilitoa tuzo dhidi ya Tanesco kuilipa Dowans shillingi billion 94. Jambo hili liliibua hisia na hasira miongoni mwa wananchi kwa kulalamika na kupinga ulipaji huo wa fedha za umma kwa kampuni tata - kutokana na taarifa za kamati teule ya Bunge.

Baada ya tuzo hiyo watu binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mawakili wa Tanesco walipinga mahakama kuu kusajili tuzo hiyo. October 2011 Mahakama kuu ilitoa uamuzi wa kusajili tuzo hiyo na kuamuru Tanesco ilipe shillingi billion 94 na asilimia 7.5 ya gharama hizo. Hata hivyo kabla ya usajili wa tuzo hiyo, Dowans iliuza mitambo husika kwa kampuni ya Symbion Powers kinyume cha taratibu kwa kuwa kulikuwa na amri ya mahakama ya kuacha hali ya mitambo ibaki kama ilivyo. Cha kushangaza ni jinsi ambavyo Serikali ilikuwa mstari wa mbele katika kuingia mkataba wa uzalishaji wa umeme na Symbion Powers kwa gharama ya watanzania hali ikijua mitambo hiyo iko kwenye mgogoro uliopo mahakamani.

Kwa kuzingatia haya, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Asasi kadhaa za Kiraia na Wanaharakati wa Haki za binadamu tulitoa tamko tarehe 11 Oktoba 2011 kuitaka serikali kuchukua hatua ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa bila mafanikio.

Kwa kuwa serikali imeamua kudharau maoni yetu, na kwa kuwa kuna kila dalili kwa serikali kuilipa Dowans fedha za wananchi, sisi, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, serikali wakilishi za wanafunzi na raia wa kawaida wa Dar es salaam tunaitisha maandamano kwa uratibu wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu siku ya Jumamosi tarehe 29/10/2011. Kwa hapa Dar es salaam, maandamano yataanzia Ubungo, mbele ya zilipo ofisi za Makao makuu ya TANESCO hadi Viwanja vya Jangwani kuanzia saa 2:30 asubuhi.

Maandamano haya yanalenga kuitaka serikali kufanya yafuatayo:-
  1. Kutokuilipa kabisa Dowans kwa kutumia hela za walipa kodi wa Tanzania.
  2. Itoe maelezo ya kina kwanini ilipuuza ushauri wa kisheria wa kuvunja mkataba na Richmond toka awali kwani kwa mujibu wa washauri wa kimarekani Hunton & Williams LLP wakati Tanesco inaingia mkataba na Richmond Dev’t Co. Kampuni hiyo haikuwa imeshasajiliwa achilia mbali kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake chini ya mkataba huo.
  3. Itekeleze kwa dhati maazimio 23 yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mlolongo mzima unaopelekea mpaka sasa tutakiwe kulipa bilioni 111. Kwa kufanya hili Serikali pia ituthibitishie kuwa itaacha kabisa kukikosea heshima chombo ambacho ni kisemaji na wakilishi cha wananchi kupitia wabunge.
  4. Kama sheria za kimataifa zinatubana kulipa deni hili basi malipo haya yafanyike kwa kuuza mali za wale waliotusababishia kadhia hii na kwamba malipo ya kuilipa dowans yafanyike pale tu serikali itakuwa imeshawachukulia hatua kali wahusika wa kadhia hii. Umma ni lazima ujiridhishe kwa kuona hatua hizo zinachukuliwa.
  5. Kuchukuwa hatua ya kinidhamu kwa wale wote walioshiriki katika kuingiza serikali katika mkataba huu hata mawakili waliotoa ushauri huu.
  6. Serikali ipeleke Bungeni muswada wa utaratibu mzuri na sahihi wa kushirikisha wananchi na hata wabunge katika kuingia mikataba ya kimataifa na serikali ili kuepusha hali kama hii kutokea.

Kwa hiyo tunatoa wito kwa watanzania wote tuadhimishe kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kutenda yafuatayo:-
  1. Tujitokeze kwenye maandamano ya amani na kupinga ufisadi na malipo ya kifisadi ya Dowans siku ya Jumamosi, tarehe 29 Oktoba 2011.
  2. Kuvaa nguo za maombolezo, nyeusi, kama ishara ya maombolezo tukikumbuka msimamo wake wa kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa,
  3. Tuzitumie siku za ibada za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili zote ndani ya muda huu, kumuomba Mungu atujalie Uzalendo na Ujasiri wa kuitetea nchi yetu, kama alivyofanya Mwalimu Nyerere,
  4. Kuwasiliana na wanaharakati nchi nzima mahali walipo, ili kupanga na kuandaa mahali pa kukutania siku ya maandamano haya ya amani.

Mwisho, tunaomba walipa kodi (wananchi) wote ambao hawajapendezwa na mlolongo huu unaopelekea ulipaji wa deni hilo la Dowans na ufisadi mwingine wote kuwa na uthubutu na kujitokeza kwa wingi kusimamia kile ambacho wanaona ni haki na stahili ya wananchi wote na taifa letu kwa ujumla.

Taarifa Hii Ilisomwa mbele ya Waandishi wa Habari na Mussa Billegeya, Marcosy Albany na Harold Sungusia kwenye Ofisi ya Legala and Human Rights Center (LHRC) – LEO Jumatano tar. 26 Oktoba 2011.

Monday, October 10, 2011

Oyaa...UDsm msituzingue!

Uongozi unapolewa sifa na waongozwa na hutaka sifa? Bila shaka sivyo....lakini ndo maisha yetu ya sasa.

UDASA sasa wana mpango wa kumtunukia Rais J Kikwete shahada ya udaktari kwa mchango wake wa kupunguza malaria.

Prof. mmoja anauliza: ni nini hii lakini?
Anajibiwa kuwa wameleta vyandalua vya bure kila kaya.
Mmoja anauliza: mbona mimi hivyo vyandalua vya bure havitoshi kwenye kitanda cha watoto achilia mbali cha kwangu?

Anapewa jibu: solution ni wewe kupunguza ukubwa wa kitanda! Ama!!!!

Mmoja amefunguka: acheni kujikomba...kama ni mchango wake kwenye afya wanaostahili kumpa ni Muhimbili ambao kwa kumbukumbu zetu tayari keshapewa. Kwa nini ninyi mumpe nyingine wakati si eneo lenu?


Nabaki na maswali: kujikomba? Ili iweje? Ili mpate consultancy serikalini?


Mmmmmh....maisha bongo bana!

Friday, October 7, 2011

Tafakari!

Bungeni huwa wanasema 'naomba ku-declare interest'! Nami nasema "mimi si mhubiri kwa kuwa upadre ulinishinda-vinginevo nami sasa ningekuwa mtakatifu kama Simon!

Katika biblia bwana Mkubwa anasema kuwa kama ibilisi akimtoka mtu na akaenda kutafuta makazi mapya naakakuta 'kumejaa' hurejea alikotoka. Na akikuta kumefagiwa na kuwa safi huzunguka huko na huko na kutafuta wenzake 7 walio waovu kuliko YEYE na kurudi pale alipokuwa na kumvagaa...(natumia lugha ya kitakatifu ya kitaa!) Na hapo ndipo aliyepagawa sasa huwa mbaya zaidi ya alivokuwa mwanzo alipokuwa na ibilisi mmoja!

Tutafakari pamoja kama taifa mustakabali wa maisha yetu kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi!

Labda hii ikusindikize weekend hii!

Wednesday, October 5, 2011

Tunatengeneza'ga' mabomu siye wenyewe?

Mtu mume na mtu mke wanapooana huwa wamejaa 'upendo' wa hali ya juu! Na baada ya hapo hata mwaka haujapita utasikia wanataka kuachana.

Nimeshuhudia mtu mke aloolewa akinunua vitu dukani anaandika jina lake. Alipoulizwa anasema 'naandika kwa jina langu kwa kuwa hujui ya leo na kesho'. Maana yake ni kuwa hajui kama ataishi mpaka mwisho wa maisha yake na huyo bwana.

Kwa maelezo yake anadai kuwa itasaidia wakati wa kugawana mali hata kama mtu mume ndo alotoa hela ya kununua hivo vitu!

Hii ni dalili ya kutojitambua na kutojiamini!

Monday, October 3, 2011

Sura tofauti...




Laiti kama sura tunazoziona kanisani na misikitini kila siku ya ibada (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) zingekuwa hivo na kuakisi ya siku ya ibada dunia ingekuwa sehemu bora ya kuishi kabisa!

Lakini...unyenyekevu wa kiibada pengine huishia hapo kwenye lango la nyumba ya ibada!

Na pengine ndo sababu tunaona yatokeayo ambayo huwa tunayatafsiri kama 'ZAMBI'.