Friday, September 30, 2011

Kifo cha PC Urassa: Mifumo mibovu inavotugharimu!








Hapa ni kijiji cha NRONGA kipo Machame juu, Mkoani Kilimanjaro

Maziko yalifanyika jana tarehe 29 mwezi huu...misa na maziko yalikuwa sambamba na mama mwingine ila yeye hakuwa askari (Domina Lema) baada ya shughuli za kuzika kawaida askari 6 na kiongozi wao jumla 7 wakacheza gwaride lao na kufyatua risasri tatu hewani kumuaga mwenzao PC Meshack Urassa ambae kituo chake cha kazi kilikuwa Mbeya na alianza kazi 2009.

Maelezo ya askari wenzake walisema amefikwa na mauti baada ya kuvamiwa na majambazi na kupigwa na kitu kichwani..inahisiwa ni nondo zinazotawala huko Mbeya.


Askari waliwasilisha michango yao kwa wafiwa...askari wenzake marehemu, wa huko Mbeya walichanga milioni moja ikakabidhiwa pale makaburini, pia kulikuwa na michango mingine huko Mbeya zaidi ya milioni 2, baadhi zikatumika kufanyia safari na zikasalia laki 9 na nusu nazo zikakabidhiwa kwa wafiwa........




Nini sababu ya NONDO huku na huko? Mifumo mibovu!

Wednesday, September 28, 2011

English Please!

Aaaah....labda kuna siku tutakuwa wakoloni ama waswahili kiuhakika!

Monday, September 26, 2011

Swali

Hivi sisi ni masikini wa nini vile?

Friday, September 23, 2011

Yaani mnazidiwa akili hata na Dereva?


Mwanafalsafa Albert alikuwa na dereva. Kisa cha yeye na dereva ni kama hivi!

"The story is that Albert Einstein's driver used to sit at the back of the hall during each of his lectures, and after a period of time, remarked to Einstein that he could probably give the lecture himself, having heard it several times.

So, at the next stop on the tour, Einstein and the driver switched places, with Einstein sitting at the back, in driver's uniform.

The driver gave the lecture, flawlessly. At the end, a member of the audience asked a detailed question about some of the subject matter, upon which the lecturer replied, 'well, the answer to that question is quite simple, I bet that my driver, sitting up at the back, there, could answer it..."

Boss wake alielezea vema kwa kuwa ndiye mwenye uelewa nalo. Wasikilizaji walisema: kama Dereva anaweza kujibu namna hiyo basi Professor ni zaidi.

Ktk nchi hii tumekuwa na akina Albert wetu wengi tu. Mwalimu Nyerere ni mmojawapo. Na yeye amekuwa na madereva/wanafunzi wake wengi tu...

Kinachoshangaza sasa ni kuwa hao madereva/wanafunzi wake wameshindwa hata kutoa mhadhara wa maana kuhusiana na nji yetu(kutatua matatizo yanayotukabili).

Ndio maana kila siku wanaimba tu...kwa nini hatujui kwa nini Tanzania ni masikini!!!

Yaani wanazidiwa kufikiri na dereva!!! Ama ndo style ya kufikiri kwa kutumia masaburi? Khaaa!





Wednesday, September 21, 2011

Eti Mali ni ya mwenyewe?

Inaonekana kuwa mara baada ya kufa mfanyibiashara mkubwa basi aghalabu biashara hiyo huenda sawa.

Hivi majuzi nilipanda moja ya mabasi mabasi ya safari ndefu ambayo wakati wanaanza safari zao ilikuwa na huduma mbalimbali kama za kutoa maji, kuonyesha sinema/video, pipi, biskuti nk.

Huduma kwa wateja pia zilikuwa safi ambapo mlikuwa mwatangaziwa mlipofika na kadhalika. Nilishangazwa na hali ya sasa ya basi hili na nilipouliza nkaambiwa...'huna habari? Mwenye mali keshakufa so watoto ndo wanaoendesha kampuni'

Swali: kwani mwenye kampuni asipokuwepo ndo mambo yaende ndivo sivo?
Je yawezekana yatokeayo Tanzania kwa sasa ni kwa kuwa mwenye mali-Mwl. Nyerere-hayupo? Je kuna siku nasi biashara ya kulinda rasilimali zetu na kuiongoza nji vema ikawa swafi kama biashara nyingine?

Monday, September 19, 2011

Dereva alikuwa katika hali gani?

Wakifanya utambuzi kwa kuangalia picha

Mara nyingi tumeona, kusikia na hata siye wenyewe kuwa waathirika wa ajali mbali mbali. Na inapotokea ajali nndipo mchawi anapotafutwa.

Hivi karibuni, baada ya ajali ya basi iliyotokea Dodoma SUMATRA ilitangaza kuifungia safari kampuni ya mabasi ya Moro Best. Baada ya wiki moja ya tangazo moja ya basi la kampuni hiyo lilipata ajali na kuua na kujeruhi watu kadhaa.

Swali: Nani wa kuwajibika?
Suala la uwajibikaji ni gumu kwa kusema ukweli hapa kwenye Tanzania yetu. Na matokeo yake serikali inajivua uwajibikaji inawatupia lawama na mzigo kwa dereva.

Hili la meli pia limekuja na kutushika pabaya. Ni kwamba SUMATRA (kama inafanya kazi Zanzibar) ama chombo kama hicho huko Zenji hakipo kuangalia usalama wa abiria na mizigo yao ama kipo kwa matakwa/maslahi yao binafsi?

Sasa msako wa Nahodha wa meli tena kwa 'uchungu' ufanywao na polisi si kitendawili? Kwani hawakuwepo bandarini na taarifa zao za ki-intelijensia?

Dereva/nahodha alikuwa ktk hali gani haina maana sana kama mifumo ya udhibiti, ufuatiliaji na kuchukua hatua haifanyi kazi (kama ipo) ama haipo!!


Friday, September 16, 2011

Helooo….Prontoooo!

Tafadhali andika press release kukanusha kuwa hakukuwa na mtafaruku/mafarakano kati yetu! Maana naona hawa jamaa wametuandama!

Heloo! Hebu andika waraka kukanusha hili kwamba hujawahi kunipa suti! Haki ya mama mwaka huu ntakomaje?

…..and the story goes on!……..



Muwe na weekend njema!

Wednesday, September 14, 2011

Hizi Data Mnazitoa wapi?

Akitoa taarifa kwa Rais wa JMT, Waziri Kabaka alimweleza mkulu wake kuwa wametengeneza ajira milioni 1.3 na ushei hivi. Kwamba serikali ilitengeneza ajira laki 2 na ushei wakati sekta rasmi ilitengeneza ajira milioni 1.1 na ushei hivi.

Swali: hizi data mnazipata wapi? Mwaka 2006 baada ya serikali kuwa madarakani kwa mwaka 1 walishirikiana na ILO kufanya tathmini ya ajira zilizopo, fursa na kuweka mikakati ya namna ya kutengeneza hizo ajira na viashirio. Mtaalam kiongozi toka India alishirikiana na wenzake toka Tanzania na kila ofisi walipokwenda waliambiwa kuwa watapewa ushirikiano.

Ulipofika wakati wa kukusanya taarifa, kila idara/kitengo walichokwenda walipewa jibu la ‘sisi hatukuwepo kabla, labda muoneni fulani/idara ya….kwa kuwa tulikuwa chini yao’. Mwisho wa siku wakajikuta kuwa taarifa waliokuwa wakiitafuta ilikuwa inapatikana kwa Rais ambaye hata wangemfuata kumhoji angewaambia ‘labda mkamhoji Rais alonitangulia kwa kuwa mie ni mgeni hapa’…Mhindi wa watu akapanda ndege kurudi India.

Sasa, hizo data za ajira 1.3m mmezipata wapi? Poleni sana!!!!

Monday, September 12, 2011

Nchi ya Voda fasta!

Kesho PM anaanza ziara ya Kiserikali mkoani Mara

Pinda

Wakati wa ziara yake tutashuhudia haya!

msafara

Kwa siku jana na leo tunashuhudia barabara ya kutoka Bweri kwenda mjini ikizibwa viraka!

Swali: hakukuwa na hela mpaka PM aje ziarani ndo mabonde yazibwe?

Kama zilikuwepo kwa nini matengenezo hayakufanyika? mambo yanafanywa ki-voda fasta tu!

Akiwa Mkoani hapa atakagua miradi ya ‘maendeleo’ na kuweka ma-JIWE ya msingi ya miradi ya maendeleo!!!!

Kisha tutaona akipokea taarifa ya serikali na taarifa ya CHAMA toka kwa mkuu wa mkoa wa hapa!!

Pale uwanjani tutaona watakaompokea wakiwa kwenye sare ya NJANO na KIJANI wakati amekuja kwenye ziara ya kiserikali!!!

Halafu huyu ndo atatoa mchozi akisema uzalendo umetoweka!!

Pole!

Friday, September 9, 2011

Ujumbe wa Leo

Si mbaya! Je majirani zako wasipokusalimia UTAHAMA mtaa ama kijiji?

Unadhani wasipokusalimia watakuzuia kufanya ama kuendelea na lile ulokuwa ukilifanya?

 

Muwe na weekend njema!!