Friday, August 5, 2011

Ziwa limetuliaaaa!

DSC03151

DSC03162

Kutoka Kigongo kwenda Busisi na kurudi kwa kivuko (pantoni) utajionea mandhari nzuri kama hii!

Wednesday, August 3, 2011

Kwenye Utajiri lakini madhila kibao

Hapa ni kwenye kisima cha Lwenge chenye kutoa maji yanayotumika ktk mji wa Geita. Wadosi wanapata maji kutoka kwenye pump inayotoa maji hapo lakini walala hoi wanajipanga foleni kuanzia saa 10 usiku. wengi wao ni akina mama-fikiria hatari zinazowakabili.

 

Pata taswira Sad smile

 

DSCF0037[1]

 

DSCF0038[1]

Maji yametoka Ziwa Victoria kwenda Kahama Shinyanga lakini yaliyoko km 45 tu toka hapa mjini imekuwa kesi! Dah!

Monday, August 1, 2011

Nani wa kutupumzisha?

Wenyeji wanayaita MAGWANGALA…masalia ya mawe toka mgodini (waste rock) yanayouzwa kwa kiroba sh 4000-5000. Kisha huletwa hapa Nyankumbu kwa ajili ya kupondwa, kusagwa na kisha kuoshwa na kupata dhahabu.

Wapondaji ni nani? Wengi ni akina mama na watoto! Ukitaka kujua ama kuona utumikishwaji wa watoto…njoo hapa utajionea.

Pata taswira Sad smile

102_0605

Afya za wanawake, watoto na vijana zi mashakani!

DSC03113

 

DSC03114

 

DSC03121

 

DSC03119

Ukifika pahala hapa na ukasikia kelele za ‘krasha’ hapo utadhani ni boeing inaondoka uwanjani! Sad smile