Friday, July 29, 2011

Uwekezaji ama ni Wizi uuao?

Kijana huyu ni mmojawapo wa wahanga wa udhalimu wa wawekezaji.

Ana miaka 13, na hajawahi kuona darasa la pili. Alisoma darasa la kwanza na baada ya wazazi wake kufia kwenye ‘kambi ya wakimbizi wa ndani (Internally displaced persons-IDPs)’ hapa Geita akalazimika kuacha shule ili kumtunza bibi/nyanya yake. Anatamani aanze shule hata kama ni chekechea Sad smile

 

102_0560

Mpaka lini haya yataendelea?

Tuesday, July 26, 2011

Nani atulilie tusikike?

Wiki ilopita Viongozi wa dini kutoka Norway, Canada, Botswana, Afrika Kusini na Zambia waliungana na wenzao wa Tanzania (TEC/BAKWATA/CCT) kutembelea wahanga wa uhalifu unaotendwa na wawekezaji kwa kuungwa mkono na serikali katika mgodi wa North Mara na Geita. Leo ninakumbushia tu stori ya watu wa Geita. Hii story haikuanza leo bali miaka kadhaa ilopita. Viongozi wa dini wameweza kuiweka ktk kumbukumbu na waweza kuisoma hapa na kuiona hapa.

102_0579

Usiku wa tarehe 31 July 2007 ni usiku wa kukumbukwa kwa wengi ktk kaya zaidi ya 80 za kijiji cha New Mine wilayani Geita. Walivamiwa usiku wa manane na polisi, wakafurushwa na kisha nyumba zao kuchomwa moto. Pamoja na kutafuta haki na kupewa mahakamani serikali yao imewaacha kuteseka kwenye mahema bila msaada!

102_0565

102_0566

 

Leo hii wako kwenye mahema kama vile hakuna serikali.

102_0550

Hili ni jengo la mahakama ya ardhi ambapo familia 86 zilitupwa usiku wa 31/7/2007 bila kujali kuwa kuna wazee, watoto na wakwe zao.

Na haya ndo mahema wanayoishi kwa zaidi ya miaka 4. Mpaka sasa kuna watoto kadhaa wamezaliwa ktk mahema haya. Mmoja wa viongozi wa dini aliuliza: je kila familia inayoishi hapa ina redio? Ni swali la kijinga linaloonekana kana kwamba linawasimanga hawa watu lakini nikakumbuka stori ya wanaoishi maeneo ya mabanda (slums) huko nairobi kwamba: ili baba na mama wakutane kimwili husubiri treni inapopita hapo na fasta fasta baba humrukia mke na humaliza shida zao wakati treni inapita!!!  Kwa hiyo kwa jinsi mahema yalivo….unapata picha!!!!!!!!

 

Pata taswira Sad smile

102_0590

 

DSC03082

 

Vyoo wanavotumia ambavyo hawakupewa na serekali bali viongozi wa dini

DSC03062

 

102_0592

 

Kwa sasa ziko familia chini ya 30. Usiniulize sasa hivi zile zingine zaidi ya 50 ziko wapi…lakini siku moja nitaibuka na jibu!

Thursday, July 21, 2011

Unapokataliwa ndani ya nchi yako mwenyewe….ni shughuli!

Huwa inashangaza sana kusikia kauli za viongozi wa nchi yetu katika ngazi mbalimbali. Jana wakati ujumbe wa viongozi wa dini (CCT/BAKWATA/TEC) wakiwa na wenzao toka Afrika Kusini, Botswana, Zambia, Canada na Norway walipomtembelea mkuu wa wilaya ya Tarime kabla ya kutembelea eneo la Nyamongo palipo na mgodi tata wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya Barrick toka Canada Mkuu wa wilaya ya Tarime Lt. John Henjewele aliwaambia viongozi hao wa dini kuwa Tarime ni sehemu ya kipekee. “katika utafiti tulioufanya tumegundua kuwa hawa wenyeji wa wilaya hii si wa Kenya wala wa Tanzania bali ni wa Tarime! Hawa watu ni ungovernable kabisa!”

 

Swali: kuna nchi ndani ya nchi katika Tanzania?

Kama hao wakurya ni ungovernable Henjewele anapaswa kurejesha fedha anayopokea kama mshahara kwa kuwa hafanyi kazi.

Wakati tunasubiri bwana mkubwa amuondoe David Jairo nadhani huyu wa Tarime anapaswa kuondoka sasa kwani ameshindwa kufanya kazi alopewa!