Thursday, June 30, 2011

Yes! Na bado

269174_202032436513513_100001202752817_619029_6367277_n

Wakimaliza ndo akili itarudi!!

Friday, June 24, 2011

Sitashangaa hili likitokea!

 

Kalonzo na JK (si picha ya Malaysia)

Tarehe 17 June mwaka huu, Makamu wa Rais wa Kenya (Stephen Kalonzo) ametoa kauli ya kushangaza (kwangu).Ndugu Steve Kalonzo alisikika katika eneo la Tiganya wakati wa hafla ya kuchangia fedha shule moja ya upili kuwa ‘ataongea na Rais wa Tanzania, JK, ili Tanzania iruhusu biashara ya MIRAA ama MIRUNGI iruhuhusiwe kuuzwa Tanzania.

 

Ikumbukwe kuwa mirungi ni zao ambalo liko kwenye kundi la madawa ya kulevya kama bangi ambalo limepigwa marufuku kulimwa na kutumika nchini.

 

Wiki hii Kalonzo ameonekana na JK kwenye picha wakiwa wanateta walipokuwa nchini Malaysia.

 

Ndiyo aina ya viongozi tulio nao Afrika wenye kusema ujinga wa aina yoyote na ukakubalika!!!!

 

kazi ipo!

Sunday, June 19, 2011

Leo Ni Siku yangu ya kuzaliwa!

Nimetimiza miaka kazaa...Nawashukuru wale wote ambao waliweza kuwa nami ktk safari ya maisha mpaka sasa.

Nawashukuru wana-blog wenzangu kwa ushirikiano.

Karibu!

Friday, June 10, 2011

Weekend Njema!

Jameni mie bado naserebuka! Huo ulaji wa Mkulo kwa sisi Matrafiki si kidogo (notification mpaka 300,000/)

Tuwemo!

Thursday, June 9, 2011

Ulaji huo!

Kama kweli makosa ya barabarani yatatozwa shilingi elfu hamsini (50,000) basi mimi kama askari wa usalama barabarani naona raha sana kwani utajiri uko bwerere kwangu! Nitabambikiza makosa hata yasokuwepo na hivo kama wewe una makosa matatu ukinipa elfu arobaini (40,000) tu nakuachia. Nikikamata gari lako tu moja kila siku kwa mwezi najihakikishia kuwa na sh 1,200,000/ ambazo ni sawa na mshahara wa katibu wa CCM Taifa!

 

Aksante Mkulo!

 

Ngoja niserebuke kidogo!

Friday, June 3, 2011

Walioelimika, Aibu iko wapi?

Watumishi wa umma ambao hawautumikii umma, bali wanajitumikia wao wenyewe

 

Wanasiasa wanaozungumza, lakini hawasemi lolote

 

Wapigaji kura ambao wanapiga kura, lakini hawamchagui mtu yeyote

 

Walimu wanaofundisha ujinga

 

Mahakimu ambao wanawahukumu watu na wanachukua mlungula

 

Wanajeshi ambao kila wakati wako katika mapambano na watu ambao inabidi wawalinde

 

Maaskari ambao hawawezi kuzuia uhalifu kwa sababu wako “busy” na mikakati ya kufanya uhalifu

 

Watu ambao wanazitumikia pesa

 

Wacha Mungu ambao badala ya kumhubiri Mungu kwa ajili ya mbingu wanamhubiri Mungu kwa ajili ya tamaa zao

 

Madaktari ambao badala ya kuokoa maisha, wanayamalizia

 

Makandarasi ambao wanatengeneza majumba yanayoporomoka na barabara zenye mashimo

 

Wafanyabiashara wanaouza takataka

 

Watu wafundishao maadili lakini wao wakiwa hawana maadili

 

(Credit: Dr Kamanzi, A)

Pata Uhondo toka kwa Mjomba!