Saturday, May 28, 2011

Jambazi anapokuwa Mtamu?

Inashangaza pale ambapo wale walouawa na polisi wanaoelezwa kuwa majambazi na wavamizi kwenye mgodi North Mara wanapokuwa wazuri machoni pa serikali.

 

Inakuwaje serikali kugharamia maziko yao hata kutoa ubani?

 

Inashangaza kwa kweli!

Monday, May 23, 2011

Mwisho Wa dunia….Mmesalimika?

Jambo wadau…nimekuwa kimya na kidogo kidogo ninarejea….

 

Sina shaka kama hamko mbinguni kama mimi (nilinyakuliwa siku ile ya jumamosi) basi mko hapa hapa!

 

Nimeelezwa kwa zoezi la kupeleka watu mbinguni limesitishwa mpaka baadaye hasa baada ya kupanda kwa gharama za chakula na pia mafuta (kwa ajili ya kuwachoma wadhambi)!

 

Basi na tuwemo! Dunia mpya ndo hii mnayoiona baada ya jumamosi!