Thursday, April 28, 2011

Ole wenu Mnaoua watu!

Wiki ilopita nimemzika mwanangu, rafiki, mpwa na kipenzi changu, Domitila. Ni mtoto wa mdogo wangu wa kike alokuwa na miaka 14 na alizaliwa akiwa na tundu kwenye moyo wake.

Juhudi zilifanyika kumpeleka India lakini waNENE walitaka kitu kidogo ambacho ni kikubwa mara 100 toka wa wazazi wa marehemu ili awekwe kwenye orodha ya watakaokwenda India!

Matokeo yake mtoto huyu ameishi kwa madawa kwa kuhudhuria kliniki ya wagonjwa wa moyo mpaka alipopoteza maisha yake jumatano ilopita huko Bugando Mwanza.

Kama vile ambavo watoa mimba huota watoto wao wakiwauliza ndotoni kwa nini waliwaua iko siku wanaopoteza maisha tokana na uzembe ama kutaka kitu kidogo toka kwa wasio nacho watawauliza!


Tuesday, April 26, 2011

Hivi tuko wapi vile?

Ukiangalia zamani ama mpaka sasa twajulikana katika vitabu kuwa tunafuata mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea!


Sasa ukiangalia kwa undani saaana utaona kuwa tunafuata mfumo UTAMAA na KUJIMEGEA rasilimali za taifa bila aibu!


Pata uhondo wenye majonzi kiduchu tu!


Sunday, April 24, 2011

Leo ni Siku ya Kuzaliwa bi mdogo Maria Fidelia

Leo ni siku ya kuzaliwa bi mdogo Maria Fidelia almaarufu Nkugi.

DSC00365

Ametimiza miaka Mitatu leo….twamuombea maisha mema na baraka tele!



Nichukue fursa hii pia kuwatakia PASAKA Njema ninyi na wapendwa wenu!

Wednesday, April 6, 2011

Ukitaka kwenda Loliondo Jiandae!

Leo nikiwa Mugumu Serengeti nimekuta watu wakiwa wamekaa makundi makundi wakisubiria magari ambayo hayajapewa vibali kwenda samunge Loliondo. Jinsi tu walivoonekana walikuwa wamejichokea hata kabla hawajafika. Pia nimekutana  na magari yakielekea Loliondo!

 

Nikiwa njiani jirani na  kijiji cha Kyandege nimekutana na basi la Bedui likitoka Loliondo likishusha mwili wa mmoja wa wagonjwa….ulikuwa umeharibika na kutoa harufu sana.

 

DSC00640

Maiti ikitolewa kwenye Buti

DSC00641

Wakiuandaa mwili tayari kuuweka kwenye jeneza

 

Pamoja na haya machungu nilokutana nayo pia nimeshangaa watoto ambao walipaswa kuwa shule wakichunga ng’ombe na kuunza maziwa barabarani!

DSC00639

Taswira…Robben Island!

DSC00552

DSC00553

Boti ya kuwapeleka watalii Kisiwa cha Robben! Ni mwendo wa dakika 30 toka eneo la Waterfront, Cape Town

DSC00560

Nikiwa na Mkuu was Kanisa la Anglikana Tanzania Akofu Mkuu Valentino Mokiwa tukielekea Robben Island

DSC00569

Twakaribia

DSC00581

Selo ya kwanza ya kufikia wafungwa enzi hizo na iliweza kubeba/kukaliwa na watu 60. Dr Kassala akiuliza swali kwa guide ambaye naye alishawahi kufungwa hapo kwa miaka mitano

DSC00582

Menyu kulingana na daraja…hii ni kwa waafrika na wahindi/colored

DSC00575

Mojawapo ya maeneo ya wafungwa kufanyishwa kazi ngumu(quarry). Tundu linaoonekana ndimo walijihifadhi kwa kuepuka jua na kujisaidia…ktk mtindo wa ‘utajiju’.

DSC00589 Hapa ni kwenye chumba cha Mzee Madiba…aliishi humo miaka 18 kabla ya kuhamishiwa kwenye jela nyingine huko Cape Town kwa miaka 9 wakati mazungumzo yanafanyika ambayo yalipelekea yeye kuachiwa huru.

Safari yoyote ile iwe ya ukombozi ni ngumu. Cha muhimu hakuna kukata tamaa.

Maji Ni Dawa!

Kuna baadhi yetu hawapendi kunywa maji…utakuta mtu anamaliza siku kadhaa bila kunywa maji!

Nakusihi, kunywa maji kwa kadiri uwezavyo!

Monday, April 4, 2011

Tunajiandaaje?

Hivi karibuni yametokea matetemeko ya ardhi huko Ujapani yakiambatana na sunami na kusababisha mafuriko na kinu cha nyukilia kuvujisha mionzi….

Mwezi wa pili mwaka huu 2011 nilipata fursa ya kutembelea mtambo wa nyuklia wa kuzalisha umeme huko Cape Town Afrika Kusini. Tulielezwa kuwa wanazalisha umeme zaidi ya 40,000mW na wanatarajia kujenga vinu vingine.

DSC00476

DSC00484

DSC00485

DSC00488

Taswira za ziara ya kutembelea kinu cha nyuklia.

Hapa kwetu huko Bahi, Manyoni, Njombe na Namtumbo kumegunduliwa madini ya Uranium ambayo yanatumika kwenye hivi vinu. Tumejiandaaje kukabiliana na athari zake? Tayari tumeshaona wakubwa wakifurahia uwepo wa madini haya bila kujali athari zake kwa watu kiafya na mazingira.

Kama tunashindwa ktk madini mengine ya dhahabu tutaweza kweli kweye hili?

Friday, April 1, 2011

Tunayo safari Ndefu

Bado najiuliza uongozi hapa kwetu unatafutwa kwa ajili gani. Imekuwa sasa kama kasumba….Maraisi wawili wakihojiwa na waandishi wa habari wa nje wamekiri kuwa hawajui kwa nini Tanzania ni maskini. Sumaye akitoka Harvard naye akadai kuwa kwa miaka 10 alokuwa waziri mkuu hakujua kwa nini tuko maskini….na kwa vile ametoka huko sasa anajua.

Wiki hii Pinda naye kasema hajui.

Tunayo safari ndefu….