Kwa muda sasa watu wa kawaida wakiwemo wanasiasa wamekuwa wakitoa zigo la lawama kwa TANESCO, ATCL, TRC ama TAZARA kwa utendaji wao mbovu.
Hata hivyo watawala wetu manyang’au ndio wa kulaumiwa kwa uozo huu kwani kwa makusudi mazima wamedhoofisha mashirika hayo ili kujitengenezea ulaji. Hivyo inashangaza sana wanasiasa wanapolaumu mashirika hayo kwa utendaji wao ilhali kwa namna moja ama nyingine wana mkono wa dhuluma dhidi ya wananchi wa nchi hii.
Umeme: Tunao wataalamu ambao wamesomeshwa na Mzee wa Mwitongo katika nyanja za ‘geothermal’, wind na ‘solar’ na kubobea katika fani hizo. Ikumbukwe maji moto (geothermal) yanapatikana ktk ukanda wa bonde la ufa (rift valley); upepo tunao mwingi tu wa kutosha na jua ni la kumwaga bila chenga! Huko Songwe kwa mfano kiwango cha geothermal kilichopo kinaweza kuzalisha 300mW! Wataalamu wetu hawa wamebaki kungoja kuhudhuria semina, warsha na mikutano ya kimataifa ilhali walichokisomea kipo. Bonde la Stigler gorge linaweza k,uzalisha zaidi ya 2000mW lakini plani ya mzee mchonga ilichakachuliwa na wakubwa wakaamua kujenga Kihansi.
TAZARA, ATCL, na TRC: kama ilivyo kwa umeme uchakachuaji wa mashirika hayo pia umedhoofisha utendaji wake. Wakubwa siku zote wamekuwa wakiingilia utendaji wao ili wao waweze kunufaika.
Ili wakubwa waweze kunufaika wameamua kung’ang’ania juu ya majenereta ya kuzalisha umeme kwani huko ndo kwenye dili. Hali kadhalika tumeshuhudia ongezeko la mabasi ya kwenda mikoa ilokuwa ikihudumiwa na reli na ndege. Mabasi hayo pamoja na malori ya mizigo yanamilikiwa na wakubwa wetu! Mbunge mmoja wa huko Rukwa kwa mfano ameingiza magari makubwa matano (semi-trailers) kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo.
Hivyo tunapojadili upandaji wa gharama na hali ngumu ya maisha wanasiasa/watawala wanaosingizia kupanda kwa MAFUTA ni UJINGA na WIZI mtupu!