Sunday, February 27, 2011

Barabara zetu..mmh!

Barabara ya Kibiti-Lindi ina mtihani na hasa kipande cha km 60 toka eneo baada ya daraja la Mkapa mpaka jirani na Somanga kimedumu katika matengenezo kwa miaka zaidi ya 5. Sijui ile ndoto ya kutoka Mwanza hadi Mtwara kwa taxi itatimia lini!

DSC00606 Mabasi zaidi ya 20 na malori 30 yakiwa yamekwama eneo la Marengero kilometa kadhaa kabla ya Somanga

DSC00607Barabara iko chepechepe

DSC00608

Katika kupishana lori ‘semi trela’ limeramba kioo cha Hiace

 

DSC00619

Ikabidi tufanye harambee ya kuondoa gogo barabani tuweze kupita la sivo tunalala hapo

DSC00625

Kufika hapa Nangurukuru (yalipo makutano ya kwenda sehemu mbalimbali kama ionekanavyo hapo kwenye bango) ni kasheshe na faraja pia!!!

Saturday, February 19, 2011

Mining Indaba-Kama genge la G-8

Kwa takribani wiki moja na ushei sikuwepo hewani hapa kijiweni. Nilikuwa Cape Town, Afrika Kusini ambako kulikuwa na kusanyiko la wakuu (CEOs) na wafadhili wa makampuni ya madini duniani ambako walikutana kwa siku kadhaa kujadili mambo yanayohusu uwekezaji ktk sekta ya madini na hasa ktk bara la Afrika. Kusanyiko hili hujulikana kama Mining Indaba.

 

Mwaka jana kusanyiko hili lilikuwa na washiriki 4000 lakini mwaka huu kulikuwa na washiriki zaidi ya 6000 wakati kukiwa na makampuni ya uchimbaji madini zaidi ya 2000 toka kote duniani.

 

Ili kushiriki na hao wakubwa ilikupasa ulipe Rand 15,000 ama dola za kimarekani 2400. Bei ya ushiriki kwa makampuni pia ni tofauti. Mazungumzo yao 95% ni juu ya namna watakavyopata faida, asilimia 4.6 ni namna wanavosaidia jamii (corporate social responsibility) and asilimia 0.4 ni jinsi uwekezaji wao unavoathiri mazingira na baioanuai! Kwa kifupi walikuwa wanazungumzia “how to capitalize the profits and socialize the costs”!

 

Serikali yetu iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Madini, Kamishna wa Madini na Mkurugenzi wa STAMICO! Serikali yetu ilikuwa na banda lakini halikuwa na taarifa zozote hivo manake ni kuwa wamelipia bure.

 

Jamani, wakubwa hao wanasema kuwa Ulaya, Marekani na Australia wameweka sheria na sera zinazowabana….. hivyo tumaini pekee ni Afrika ambapo hakuna sheria na sera za kuwabana na hata kama zipo wanaweza kuwabana viongozi wa serikali wakazibadilisha ili kuwaneemesha wao!!

 

Kaazi kweli kweli!

Friday, February 18, 2011

Poleni sana

184277_188361657863708_100000696254336_536909_7097881_n

Napenda kuwapa pole wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wameathiriwa na matukio ya mabomu ya Gongo la Mboto mnamo usiku wa kuamkia jana!

Thursday, February 3, 2011

Kazi Ikigomba unapumzika tu!

Machinga wamelala jirani na benki ya NMB Musoma huku wakiwa wametandaza mali zao wakisubiri wateja usingizini!

Wednesday, February 2, 2011

Ziwa letu ni chafu sana!




Ukiwa kwenye boti kuelekea Kinesi tokea Musoma maji ya rangi hiyo ndo wayaona.