Friday, January 28, 2011

Seriously: Mnambie kwa nini nijiunge na mifuko ya akiba uzeeni!

Inasemekana kuwa mifuko ya akiba uzeeni kama vile NSSF, LAPF, PPF nk inamsaidia mtu/mfanyakazi kumtunzia njulugu kiduchu ili atakapostaafu zimsaidie kufa kwa heshima!

Mimi sijawahi kuajiriwa ndani ya serikali wala sekta binafsi na hivyo inapotokea kutongozwa niajiriwe najiuliza na kuwauliza nitapata nini naambiwa pamoja na 'mazuri' nitakayopata ni kulipiwa 10% ya mshahara wangu na mchango wangu kwenda mifuko ya akiba uzeeni nitakayochaguwa mwenyewe.

Hapo ndipo ninakuwa na kigugumizi kabisa kwa sababu kubwa zifuatazo:

  1. Wazee wanapostaafu husotea sana hicho kidogo ambacho wamekitunza huko 'mfukoni'. Akiba ina shilingi milioni 2 mstaafu anaweza tumia robo tatu ya hiyo pesa kuifuatilia!
  2. Mifuko hiyo badala ya kuonekana kama watunzaji sasa wamekuwa wanyonyaji! Kwa mfano: Kuna taarifa kuwa jengo la PPF Towers kiukweli thamani yake ni shilingi bilioni 9 lakini gharama zilizoko kwenye madaftari ni bilioni 18! Bilioni 9 zishalambwa na wajinga wachache wanaodhani jasho la mtu laliwa! Hapo Arusha kuna jengo la NSSF linajengwa na kampuni ya kichina. Jengo hilo la ghorofa 12 na basement linalotizamana na Kathedrali ya Waanglikana (St James) linakadiriwa kuwa litagharimu sh. Bil. 27!!!!! Nashangaa sana kwa kuwa ktk jiji hilo hilo la Arusha kuna hotel ya kitalii ya ghorofa 11 na basement (inatizamana na Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha) inakaribia kuisha na imeshatumia bil 8 na wakiongeza finishing na furnishing za ndani haitazidi bil 10 na inajengwa na kampuni ya kichina pia!!
Hapo ndo napatwa na kizungumkuti....kwa nini nichangie kwenye kueneza ufisadi? Halafu watu wanalipa staff/workers development levy lakini wafanyikazi hawaendelezwi!

Hebu nambie...kwa nini nichangie kwenye hiyo mifuko? Aaaagh!

Thursday, January 27, 2011

Uamuzi juu ya Matusi haya yangepelekwa katika jamii safi sana!

Inasemekana mwaka juzi mtoto mmoja wa sekondari alifutiwa matokeo kwa kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mtohani wa kidato cha nne.

Mwaka jana idadi imepanda mpaka wanafunzi wanne waliofutiwa matokeo kwa kutusi karatasi!

Mwaka huu yawezekana wakaongezeka na kuwa saba (waliongezeka watatu na kufanya idadi kuwa wanne mwaka jana)!

Baraza la mitihani limetumia kifungu cha 5 na 3 cha kanuni za mitihani na adhabu yake ni kufutiwa matokeo!

Najiuliza kama sheria zinafuatwa kwenye mambo fulani kwanini zisitumike hata kwenye siasa na jamii?

Wednesday, January 19, 2011

Kilio cha Kijinga!

Nchini kwetu sasa kuna kilio cha kijinga kuwa elimu imeshuka…yawezekana kweli elimu imeshuka. Nakumbuka nilianza kuandika barua za kiingereza nikiwa darasa la nne ktk shule hizi hizi ambazo wakubwa/watawala hawapeleki watoto wao tena.

 

Sasa hivi kumekuwa na uchuro wa shule ziitwazo ‘English Academy’ ambazo sasa zimegeuka kuwa usanii wa hali ya juu sana. St Mary’s ya ‘Dr’ Mchungaji Rwakatare si ile ambayo tuliijua wakati inaanza. Kama ilivyokuwa kwa kampuni ya mabasi ya Scandnavia Express kuchakachuliwa kwa wakubwa kuingiza mabasi yao na hizi shule zimechakachuliwa na wakubwa kuingiza shule zao wakitumia majina makubwa kama St Mary’s nk.

 

Kitendawili na kichekesho ni kuwa wakubwa wetu wanastuka kuvuta shuka wakati kumekucha.

 

Wanadai kigezo cha kupata mikopo kwa elimu ya juu ati ukiwa umesoma english medium hustahili mkopo…na ukiangalia ni kuwa wanaopata mikopo si watoto wa maskini bali watoto wa wakubwa. Kinachoshangaza ni kuwa sidhani kama kwa mtindo wa ktokuwa na mikakati ya kutengeneza ajira hakuna mpango madhubuti wa ku-track wakopaji na kurejesha hizo fedha ili ziweze kutumiwa na wengine.

Shule za umma ziiko hoi….shilingi 15,000 inayotolewa kwa kila mwanafunzi haimfikii shuleni ama inafika sh 2,000 tu baada wa wakubwa kujikatia huko juu. Matokeo yake shule zetu zinakuwa hovyo kabisa. Na wanaopeleka academy watoto wao ni hao wakubwa na akina sisi Ng’wanambiti, Matondo, Mbele, Yasinta, Da Mija Emu 3, Makiya nk!

 

Wakati wakubwa wetu wanastukia huko juu, wenzetu Kenya kuna mvutano mkali kati ya mafisadi wa elimu na serikali. Wameweka sera kuwa ili uchaguliwe kuingia sekondari ‘priority/preference’ itatolewa kwanza kwa wale waliosoma shule za umma ‘public’ na ndipo shule za academy bila kujali maksi alizopata mtoto.

 

Sasa wenye shule za academia wana wasiwasi kuwa wazazi watazoa watoto wao toka huko wawapeleke shule za umma na hapo ndo kimbembe kipo.

 

Najiuliza siye tutastuka lini?

Monday, January 17, 2011

Taarifa za Kiintelijensia zisizo na Intelijensi!

Najiuliza:

 

Wakati watu wanatoa rushwa kwenye uchaguzi intelijensia huwa haipo?

 

Mzee wa vijisenti (samahani MMN, najua huyu ni mbunge wako…lol!) anaficha hivo vijisenti huko nje intelijensia ilikuwa wapi?

 

Wakati watu wa migodi na wafanyibiashara wengine wanakwepa kodi na kubinya mapato yetu intelijensia haipo?

 

Wakati wanawake wajawazito wanalala mzungu wa nne hospitali intelijensia huwa imekwenda likizo?

 

Wakati vituo 45 vya afya hewa vikipewa ruzuku na madawa yenye thamani ya mamilioni ya fedha huko Tanga kwa zaidi ya miaka 2 intelijensia iko wapi?

 

Wakati George yule faru anauawa huko serengeti Intelijensia ilikuwa wapi?

 

Wakati wa EPA intelijensia ilikuwa wapi?

 

Naweza kuendelea mpaka mwaka 2038 nikiuliza juu ya hizi intelijensia zenu zisizo na intelijensi!

IGP Mwema unaboa!!!!! si useme tu kuwa chama dume tumekutuma?

Friday, January 14, 2011

Tutarudi kulekuleeee!

Iko hadithi moja huko umangini/uchaggani ktk mkoa wa Kilimanjaro. Kwamba kulikuwa na Mangi mmoja alieitwa Senguo (alifariki miaka ya 1945) na alikuwa akiogopwa sana. Kwa kawaida ilikuwa kwamba kila kitu kizuri anachokuwa nacho mtu (kama mbusi, ng’ombe, ndisi nk) lazima kiende kwa Mangi na Mangi huyo alikuwa na mashushu wake walioitwa Waringi ambao walikuwa wakimletea mangi habari za kiintelijensia! kama ulikuwa na kitu ambacho kilipaswa kwenda kwa mangi na hukukipeleka Waringi walipeleka taarifa na uliadhibiwa vikali mbele ya hadhara.

 

Kama ulikuwa na mbusi nzuri utaadhibiwa, kisha utachinja Mangi atapikiwa na kula na watu wake na kuondoka kwenda kwenye mji mwingine. Toka hapo angebebwa na Waringi…mijitu ya miraba minne na kwenda mji unaofuata na watu wangine wangejipanga kumsubiria huku wakisherehekea kama mazuzu!

 

Mangi alijipaka mafuta ya ng’ombe/samli na yalitoa harufu kali sana! Na wakati Mangi akibebwa kwenda misele akitaka kujisaidia haja ndogo aliachia huko huko juu na kojo kutelemka na kuwamwagikia wapagazi/waringi ambao waliamini kuwa hayo ni maji ya baraka yatokayo kwa Mangi na waliweza kukaa hata wiki nzima ili baraka zisiondoke!

 

Hadithi hii inanikumbusha yanayotokea hapa kwetu!

 

Kakikundi kadogo ka watu kanamiliki na kugawana rasilimali za nchi hii!

 

Kikundi cha watu kinatumiwa kama Waringi kunyanyasa watu na walio wengi wanapewa kanga, pesa, tisheti nk wakiaminishwa kuwa ni baraka toka kwa Mangi!

 

Kaazi kweli kweli!

Wednesday, January 12, 2011

Viwanja vya NMC!

SAM_2192

Mteremko wa kuelekea Metropole

SAM_2202

SAM_2204

SAM_2206

SAM_2210

SAM_2216

Uwanjani

SAM_2224

SAM_2225

SAM_2226

SAM_2228

SAM_2233

SAM_2235

SAM_2236

Msafara kutoka Hosp kwenda NMC

SAM_2170

SAM_2164

SAM_2172

Bodaboda wakiongoza msafara

SAM_2176

SAM_2178

Watu wakiwa kwenye msafara

SAM_2181

Gari likiwa wa wanahabari

SAM_2184

Gari lenye mojawapo ya maiti

SAM_2185

SAM_2186

Hisia na hujuma haziepukiki!

 

Mpaka sasa saa 7 mchana kuna malumbano hapa. Ndugu wa jamaa alouawa (kutoka jamii ya kiislamu) wanasemekana kugoma kupeleka mwili wa marehemu uwanja wa NMC kwa ajili ya kuagwa na wananchi waliofurika huko. Kisa? Kuna minong’ono kuwa familia ya marehemu wamepewa fedha wasimpeleke jamaa huko uwanjani!!!

Lakini habari zaidi ni kuwa maiti za walioko hospitali kutokana na kupigwa na risasi ni zaidi ya watatu na jamaa zao nao wanataka nao wapelekwe uwanja wa NMC wakaagwe kishujaa. Hivyo upande wa serikali (polisi) unajaribu kushawishi wapelekwe watatu tu ili kuepusha vurugu zinazoweza kujitokeza. (NOTE: hii si Official statement ya serikali kwani hilo suala la idadi ya walokufa inapaswa kutolewa na polisi ama msemaji wao).

Poleni sana! Hisia haziepukiki!

Utaficha yoote lakini hisia hazifichikiSAM_2145

SAM_2146

Ni zaidi ya maumivu?

SAM_2151

SAM_2152 

Kweli?

SAM_2155

SAM_2153

Nje ya Mount Meru Hospital

SAM_2121

Wazee wa CHADEMA wakijadili jambo nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha

SAM_2123

Vijana wakionesha hisia zao kwa mabango

SAM_2128

Watu kibao nje ya Mt Meru Hosp.

SAM_2130

Watu zaidi wakielekea Mt Meru Hosp.

SAM_2122

Magari ya wafuasi na wapenzi wa CDM wakijongea hosp kwa ajili ya kuanza msafara

SAM_2131

watu zaidi…

SAM_2133

Boda boda nao….

SAM_2136

Hapatoshi….

SAM_2140

Msisitizo...

HApo chini gari la wanausalama lipo japo wamejichanganya na watu

SAM_2139 SAM_2137

Nje ya AICC nako pamejaa

SAM_2140

Tuko pamoja

Arusha Asubuhi Hii!

SAM_2091

Watu wakielekea Uwanjani NMC

SAM_2094

Watu waliowahi uwanjani NMC

SAM_2095

Uwanjani saa 4.30 Asubuhi

Leo sikukuu! Ubwabwa na kila kitu!

Leo ni sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar!
Nimekumbuka sms ya rafiki yangu alonitumia kuwa:
"Enzi za Mwalimu ikifika siku ya Uhuru/Mapinduzi watu huandamana kwa nyimbo za kupinga unyonyaji, ubeberu, umbuzi na ukabaila. Walihimiza ufanyaji kazi kwa bidii na kilimo cha kufa na kupona.
Siku hizi siku ya Uuru/Mapinduzi watu wanafurahia kutokwenda kazini na kushinda katika gesti bubu na baa; wengine kukaba watu njiani. UPUUZI MTUPU"
Leo ni siku ya mapinduzi na hapa Arusha tunaaga wenzetu walopigwa na risasi na 'polisi'. Ndiyo, kwenye mabano kwa kuwa hawa ni sawa na majambazi wa kisiasa tu kwa kukubali kwao kutumiwa na wanasiasa.
Niko hapa si kwa kuwa ni mwanachama wa chama hiki bali Mtanzania! Atleast nina sababu ya kusherehekea Mapinduzi!

Friday, January 7, 2011

Ndio Bosi!

Kadiri siku zinavokwenda ndo mambo yanabadilika…

 

Kama nchi tunaacha mema yenye kutufanya tuendeleee na misingi bora tunashabikia ujinga. Leo hii kila mtu Tanzania anataka kuitwa Mheshimiwa ama Bosi! Niliwahi kuitwa kwenye mkutano mmoja ambao ulijadili namna ambavyo tutamaliza tatizo la mauaji ya Albino nchini na mgeni rasmi alikuwa Mizengo Pinda.

 

Uongozi wa mkoa ulinambia niandae risala/neno kwa niaba ya Mara…nikajipinda mwanaume…Ndugu Waziri Mkuuu bla bla blaaa! Nilipoipeleka hiyo ‘draft’ ya hotuba/risala huko mkoani wakubwa wakaondoa neno ndugu na kuweka MHESHIMIWA!

 

Nikaliacha kama lilivyo…nilipoingia kwenye mkutano nikasoma NDUGU huku nikipiga chabo kuona ‘reaction’ ya wadau wakiwemo wakuu wa protokali nikaona wananikodolea macho!

 

Swali: huu uheshimiwa ama ubosi manake nini? Je ndio sababu pengo kati ya wenye nacho na wasokuwa nacho linakuwa kubwa?

Thursday, January 6, 2011

Na Bado!

Waliwahi kusema huko nyuma, na ktk vibaraza vyetu tukaeleza kuwa amani tunayoambiwa na wanasiasa ni ya kutokuwa na vita ila MIOYONI mwa watu hakuna amani kamwe.

 

Tumeelezea kuwa suala la kuwatumia vijana wakati wa uchaguzi na baada ya hapo kuwaona maadui litakuja kuigharimu nchi hii. Matokeo yake tunaambiwa kwenye kampeni kuwa zimetengenezwa ajira milioni kadhaa kwenye makaratasi…vijana wanaendelea kukata tamaa!

 

Rafiki yangu askari aliyeko Arusha ananambia askari polisi wanaoishi uraiani wamehamia kambini na familia zao (na hivo kusababisha msongamano wa watu kambini) na kikosi cha jeshi l(JWTZ) cha Monduli wamewekwa stand-by! Na kwamba askari 300 zaidi wamepelekwa Arusha!

Taarifa kuwa kuna Askari mmoja kachinjwa na vijana wenye hasira baada ya kuishiwa mabomu/risasi ni kielelezo cha kuwa akili iliyo tupu ni hatari sana!

 

Tusubirie manake hatujui yatakayokuja!

Tuesday, January 4, 2011