Monday, November 28, 2011

Siku hizi ni kwa vichanga!



Bado tunaendeleza mila. Kuna jamii (kabila) zaidi ya 16 mkoani Mara zinazojihusisha na ukeketaji kwa watoto wa kike. Msimu ndo huu baada ya mavuno, mbali na wasichana ambao hawako tayari kutukanwa na wenzao visimani kuwa ni 'wasagane', sasa hali imehamia kwa vichanga, majumbani ama kwa kushirikiana na manesi huko mahospitalini.

Ile sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) imelala fofofo!

6 comments:

  1. Mungu wangu hivi twaendapi? Hii inazihirisha elimu isivyo elimisha.
    Kwa7bu wafanyao hivo wamesoma lkn elimu waliyosoma haikuwasaidia kitu.

    ReplyDelete
  2. Nina mabinti watatu hapa na napata wakati mgumu kuangalia na kutafakari picha hii....Ati, tumekuwa huru kwa miaka mingapi vile?

    =============>

    Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!

    http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html

    ReplyDelete
  3. ISSACH CHE JIAHDec 26, 2011 11:30 PM

    Du hii ni nomaa kwani sasa haya mambo ni magumu sana kama munawavizia vichanga pole sana
    kwaheri kaka chacha kwani leo kwa mara ya kwanza nimefungua web yako nakutana na hayo maswahibu ,kwakweli lawama sijuwi zimwangukie nani
    Issack Che Jiah

    ReplyDelete
  4. Hodi, Chacha!

    Heri ya mwaka mpya 2012 ingawa posti hii ni ya mwakajana!


    Naomba tusiwape wajinga heshima ya kwamba ujinga wao ni mila wala desturi: Ujinga ni ujinga tu na desturi zikiambatana na dini za watu ni vitu tofauti kabisa na ujinga.

    Desturi na mila ni kama mwangaza katika jamii wakati ujinga ni giza na maumivu mtupu kutokana na kujikwaa katika hilo giza.



    Mungu ameumba tendo la ngono ili liwe na utamu na mvutio wake kwa ajili ya kutiimiza amri Yake "[Mzae na mue wengi wa kujaza dunia]"


    Mwanaume kwa umalaya wake na unoko kwa vya wengine huku vyakwake akivipigia marufuku (wasipate wanaume wengine), yeye aamua "Mungu ni mpumbavu".


    Mwanaume akaamua "Yeye akiwa dume eti anataka raha ya ngono iwe ni haki yake peke yake na sio kwa mwanamke na ndio maana watoto wakike wanakatwakatwa "ili wasiwe malaya wa kuwashwawashwa hovyo hapo ukubwani".


    Itikadi hiyo mbovu ni sawasawa na ya huko India ambamo unasikia katika baadhi ya makabila wanawake "ki mila na desturi" huvishwa PURDAH au "chupi ya chuma" ili mwanamke asiwe na hamu ya kufanya mapenzi na mwanaume asie wake wakati mumewe yuko safarini huku kwa upande walo dume likiwa likifanya umalaya na wanawake wengine hukohuko ugenini!


    Wasiekielewa hao wajinga ni kwamba KWANZA:

    tendo la mapenzi si lazima huko wanakofikiria wao. Hata juu ni sawa kabisa (ORAL)!

    PILI:
    Hamu ya mapenzi haiko chini bali juu kwenye ubongo wa mwanamke. Kwa hiyo, hata ukikatakata sehemu zote unazoamini ni zenye hamu, ubongo wake kama yeye "ni malaya" lazima utahamishia hamu hiyo kwenye sehemu zingine kabisa za mwili wake HATA KWENYE MKONO WAKE ANAETUMIA KILA SIKU KUKUPIKIA WEWE MUMEWE UGALI!


    Sasa "suluhisho" lao la kumkatakata mtoto wa kike (au, kama India, kumvisha "chupi ya chuma") limeleta manufaa gani?

    "Ukeketaji" sio mila wala desturi; bali ni ushetani na ujinga wakupingana na kupigana nao sawasawa na mauaji ya waAlbino Tanzania au utekaji nyara kwa watoto wakike visimani huku kwetu Afrika Kusini!

    ReplyDelete