Friday, October 7, 2011

Tafakari!

Bungeni huwa wanasema 'naomba ku-declare interest'! Nami nasema "mimi si mhubiri kwa kuwa upadre ulinishinda-vinginevo nami sasa ningekuwa mtakatifu kama Simon!

Katika biblia bwana Mkubwa anasema kuwa kama ibilisi akimtoka mtu na akaenda kutafuta makazi mapya naakakuta 'kumejaa' hurejea alikotoka. Na akikuta kumefagiwa na kuwa safi huzunguka huko na huko na kutafuta wenzake 7 walio waovu kuliko YEYE na kurudi pale alipokuwa na kumvagaa...(natumia lugha ya kitakatifu ya kitaa!) Na hapo ndipo aliyepagawa sasa huwa mbaya zaidi ya alivokuwa mwanzo alipokuwa na ibilisi mmoja!

Tutafakari pamoja kama taifa mustakabali wa maisha yetu kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi!

Labda hii ikusindikize weekend hii!

1 comments:

  1. Umenitafakarisha aisee!
    Na asante kwa kumchomekea Mrisho Mpoto!

    Wikiendi Njema kwako pia Mkuu!

    ReplyDelete