Wakifanya utambuzi kwa kuangalia pichaMara nyingi tumeona, kusikia na hata siye wenyewe kuwa waathirika wa ajali mbali mbali. Na inapotokea ajali nndipo mchawi anapotafutwa.
Hivi karibuni, baada ya ajali ya basi iliyotokea Dodoma SUMATRA ilitangaza kuifungia safari kampuni ya mabasi ya Moro Best. Baada ya wiki moja ya tangazo moja ya basi la kampuni hiyo lilipata ajali na kuua na kujeruhi watu kadhaa.
Swali: Nani wa kuwajibika?
Suala la uwajibikaji ni gumu kwa kusema ukweli hapa kwenye Tanzania yetu. Na matokeo yake serikali inajivua uwajibikaji inawatupia lawama na mzigo kwa dereva.
Hili la meli pia limekuja na kutushika pabaya. Ni kwamba SUMATRA (kama inafanya kazi Zanzibar) ama chombo kama hicho huko Zenji hakipo kuangalia usalama wa abiria na mizigo yao ama kipo kwa matakwa/maslahi yao binafsi?
Sasa msako wa Nahodha wa meli tena kwa 'uchungu' ufanywao na polisi si kitendawili? Kwani hawakuwepo bandarini na taarifa zao za ki-intelijensia?
Dereva/nahodha alikuwa ktk hali gani haina maana sana kama mifumo ya udhibiti, ufuatiliaji na kuchukua hatua haifanyi kazi (kama ipo) ama haipo!!

0 comments:
Post a Comment