Marekani imewashtaki BP kwa kuchafua mazingira! kwetu Barrick Gold na GGM wanachafua kweupeee lakini wanapeta tu!
Mmmh! Haya, Nimeacha!
Ihayabuyaga!
Tuanze safari yetu ya pamoja kutafakari hali na mustakabali wa maisha ya Kijijini Kwetu. Haina maana ya kule nitokako bali hata kwako pia. Yawezekana huna ukakika kama sitafika! Karibu sana
Marekani imewashtaki BP kwa kuchafua mazingira! kwetu Barrick Gold na GGM wanachafua kweupeee lakini wanapeta tu!
Mmmh! Haya, Nimeacha!
Ihayabuyaga!
Mkutano wa Viongozi wa maziwa makuu wamemaliza mkutano wao huko Lusaka wakitoa azimio la kuwashtaki wazungu wanaoiba/vuna rasilimali za nchi hizo bila kufuata taratibu na bila kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo!
Nimeona picha ya video ya viongozi hao na nyuso zao zilikuwa na tabasamu la ‘funika kombe mwanaharamu apite’. Si ajabu baada ya mkutano waliwapigia mabwana wao na kusema ‘Don’t mind about the Lusaka resolution…we weren't that serious, you what am talking? Tis business as usual!’
Naacha: Ihayabuyaga
Wazee mnaohudhuria misa/ibada ya vijana ilihali yenu ipo mkichezeshwa kiduku ama simama-kaa mtamlaumu nani?
Nenda nje ya kasha/box uone uhalisia!
Naacha: Ihayabuyaga!
Taarifa toka mbugani serengeti zilizotufikia hapa Musoma ni kuwa mmojawapo wa Faru (5) walioletwa toka Afrika kusini na kukabidhiwa Rais Kikwete mwaka huu kwa mbwembwe amekutwa ameuawa na watu wasiojuilikana.
Tutawajuza zaidi!
Wiki hii serikali imeingia mkataba na African Rice kutafiti uzalishaji wa mchele ama mpunga, ita vyovyote vile! Na wanadanganywa kuwa ni mchele bora saaana utakaoondoa tatizo la chakula katika Tanzania!
Wasichojua ni kuwa shirika ama kampuni hiyo yenye makao yake mikocheni tayari ilishaanza siku nyingi huko Kyela katika eneo ambalo twaweza kuliita kitovu cha mpunga/mchele Tanzania!
Mbaya zaidi ni kuwa utafiti na majaribio si kihivyo inavosemwa bali kuzalisha mchele ambao umebadilishwa vinasaba (genetically modified rice).
Ni mchele na pengine vyakula vya namna hiyo vinavyopingwa ulaya na marekani kwwa sababu ya matumizi makubwa ya madawa na mbolea za viwandani ndio wakubwa wetu wanasherehekea juu ya dili za namna hiyo!
Tukumbuke kuwa mradi huo na mingineyo kama ile ya utafiti wa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba yanafadhiliwa na kibaraka wa wakoloni Koffi Annani kupitia mpango unaoitwa AGRA wakifadhiliwa na Gates Foundation na Rockefeller Foundation!
Hiyo yote wanatengeneza masoko ya makampuni ya mbolea na mbegu ya wakoloni kama Syngenta, Mosanto na mengineyo! Na ni moja tu ya sababu ya kuyakataa.
Wakati watu wa Ulaya na Marekani wanataka mazao yaliyolimwa kiasili (organically grown foods) siye twaendelea kufakamia GM foods. Haya na twendelee tu kuwa dampo la yasioyotakiwa ulaya na marekani…tukishamaliza rutuba ardhi yetu kwa kuiharibu kama Isimani iringa labda akili itatujia! Tukishapoteza mbegu zetu za asili na kuishia kununua na kupoteza uwezo wetu wa kushirikishana kijamii akili itarejea tu!
Soma hapa kupata sababu 12 kwa nini tukatae ujinga huu!
Naacha
Wenu: Ihayabuyaga!
Kauli ya waziri mmoja kuwa malipo ya 187 bilioni kwa Dowans ni maandalizi ya 2015 inastua na kufikirisha. Inastua na kushangaza kwa kuwa nadhani kama wakubwa wameamua kuwa wajinga wakidhani kuwa matumizi ya pesa yatakuwa ndo suluhisho la ushindi!
Sishangai hayo kufanyika kwani ktk nchi ya jirani ya Zambia kampuni moja ya madini ilimpa mgombea urais fedha nyingi tu kwa ajili hiyo. Na kwa kuwa ilikuwa nyingi kiasi hicho wakamshauri afungue akaunti Botswana na fedha ikaingia huko! Kabla ya uchaguzi pesa hiyo ikaondolewa kiasi hatua kwa hatua ikaenda Afrika Kusini kwenye akaunti ya mtoto wa Rais na na kisha kuhamishwa kwenda Zambia kugharamia kampeni!
Umafia wa namna hii ndo tunaona unatokea kwetu! Na kama asemayo huyo mkulu ni kweli wananchi wanatakiwa waamke waone jinsi wanavyoliwa kwani kama Zambia watawala hawako kwa ajili ya maslahi ya wananchi bali kwa maslahi yao wenyewe. Tunayo makampuni hapa kwetu ambayo yanafadhili wanasiasa. Mwaka 2005 CEO mmoja wa kampuni moja huko Arusha alimuonesha mwandishi mmoja nyaraka za kiasi cha fedha walizochangia kwenye kampeni zaidi ya milion 300 na akamwambia asimfuatefuate kuandika yanayotokea hapo kwa kuwa kuna baraka za wakubwa…mwandishi akaguna akapoozwa kwa tiketi ya ndege kurudi Dar na sh laki 3!
Naacha, wenu Ihayabuyaga!
Mmmh! Huo msemo aliwahi kuutumia mbayuwayu wetu! Na unanikumbusha kauli ya CEO mmoja wa kampuni moja iitwayo Paladin kutoka Australia inayochimba madini huko Malawi aliyoitoa kwa wanahisa wake ktk mkutano mkuu (AGM) kuwa ‘We are coming to invest in Africa because there is poor/weak governance zones’! Kuuuumbeeeeeeeeeee! Nshaelewa sasa kama si kulewa!
Kama haitoshi wakati wananchi wa maeneo hayo ya mgodi wakiwa hawaridhiki na yatendekayo mkulu wa kampuni hiyo akasikika kuwa ‘we will make the President a shareholder in our company’.
Hapo tunaona ujinga wetu siye wenye kufanya maamuzi ya mambo makubwa yanayowaathiri wananchi wa kawaida. Huko Uganda huwezi kuwekeza na ukawa salama bila kumhusisha kijana wa rais M7 a.k.a mzee wa Rap (do you want another rap????). Hapo kwetu unaweza kuona hata bila kuambiwa juu ya ujinga wa namna hiyo! katika miradi yote mikubwa kuanzia mahoteli mpaka vitalu vya kuwindia wanyama mbugani mikono ya wanene!!!
Na ndiyo sababu kusema ule ukweli tunahitaji kubadili mifumo ya utawala. FUNGUKA!
Ndiyo, labda ni sawa kabisa kutetea haki za Wasenge na Mashoga kuliko kutetea wananchi kwa kuwa labda unaweza kusikilizwa! mengi yanatokea na ndo sababu ukiangalia utaona kuwa watu kama Slaa na chama chake wanasakamwa kwa kudai mabadiliko ya kimifumo ktk utawala wa nchi ikiwamo katiba mpya.
Ndiyo, ndo sababu wabunge wa chadema walipotoka nje walizomewa na wenzao kwa milio ya ‘CCM! CCM! CCM!’ Sina hakika nani alikuwa akiimbiwa hayo yote na ikafuata kauli za kubeza.
Tatizo la wabongo tunajadili matukio badala ya ‘issues’! Na hata mkulu wa nchi wakati analizungumzia hilo suala akasema kuwa hao walotoka nje hawawezi timiziwa matakwa yao (walowaahidi wapiga kura) bila kumlilia! Ujinga ama ulevi gani huu?
Kijamii kuna watu wamesakamwa kwa kuwa wametetea wananchi wa kawaida na wajinga fulani ndani ya serikali na CCM yangu wakiwaambia kuwa kama wanataka waanzishe vyama vya siasa ama wakavue majoho kwenda kugombea nafasi za kisiasa!
Ni lini watawala watakapoweka maslahi ya watu mbele zaidi ya maslahi yao binafsi?
Jana ‘kampuni’ ya masuala anga za mbali kama ile ‘kampuni’ ya kimarekani ya aina hiyo hiyo iitwayo NASA (siyo Nasa kule Magu, mkoani Mwanza) imezindua mkakati wake miaka 10 wa kwenda mwezini na kuendeleza technolojia ya anga, kuweka masetilaiti nk. Uzinduzi huo umefanyika hapa Midrand, yalipo makao makuu ya bonge la Afrika!
Akihojiwa asubuhi hiyo ya jana, Waziri wa Sayansi na Tekelinalokujia wa kwa Madiba, mwanamama ngangari, nimempenda! Anajua anachokifanya na amesema hiviiii…. wanao watu (utaalamu) na teknolojia ila hawana rasilimali. Kwamba watatafuta rasilimali kwa namna yoyote ile toka kwingineko Afrika na kwamba washaainisha nchi ambazo zina rasilimali nyingi ambazo watazivuna huko!
Na kwamba wameainisha pia watakaoshirikiana nao (partnership) kuwa ni Algeria, Nigeria na Kenya! Unaona? Wavune kwetu rasilimali kwetu wabia wawe watani wetu wa jadi!
Lakini, mpaka Kenya kuonekana ni kwa kuwa wenzetu wamejiandaa siku nyingi….nakumbuka kuwa wakati mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Wangwe anuawa a.k.a kupata ajali, kuna taarifa kuwa setilaiti za Kenya zilinasa tukio hilo na kuwajulisha wahusika. Kama kawaida ripoti za matukio yenye utata kama hayo kama ilivyokuwa kwa Sokoine huwa hazitolewi!!!!
Lini siye tutakuwa na mkakati wa maendeleo ya kisayansi? Au ndo ile mineno ya watoto wote wa darasa la nne na saba hawatatahiniwa bali watapita tu mpaka basi?
Tafakari!
Leo madingi wako Cancun, Mexico!
Leo hii wakubwa wa nchi walogeuka mambayuwayu wako Cancun, Mexico kwenye mtukano wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi!!! Bila shaka mbayuwayu wetu naye atakuwapo manake nimeona hapa kwa Madiba wanaonesha jinsi mbayuwayu wa hapa alivoingia Mexico kwa mbwembwe!
Kinachoshangaza ni kuwa wanakwenda kujadili mambo ambayo wakubwa washayatolea maamuzi kuwa hawataki kutekeleza yale yote yaliyoko kwenye mkataba wa Kyoto (Kyoto protocol on Climatic Change). Kama vile malengo ya milenia (MDGs) hakuna cha maana kitakachofanyika badala yake watasaini makubaliano (declarations) na kurudi….na utamu zaidi uko pale ambapo watakuwa (wale wa kutoka Africa) wanauchapa usingizi na wakistuka wenzao watakuwa washapiga bao!!!
Baada ya muda watakutana tena kufanya tathmini ya makubaliano ambayo hayakuwa yao….Hawatakutana kujadili MKUKUTA bali hayo waloyafanya ktk nchi ya ugeni! Laiti kama wangejua! Na kwa kuwa washazoea kwenda mikutano kama si mitukano kuna watu serikalini wanahudhuria mikutano 300 ya kimataifa kwa mwaka :-(
Mtu huyo ukimtafuta ofisini hapatikani, na kuna wanaobadilishia nguo na kupewa masurufu yao airport….mmmmh! Wizi mtupu!
Habari zenu wadau! Nimepotea na yawezekana nkaendelea kupotea hewani…
Leo naomba mnisaidie maana ya KUONDOA SHILINGI ktk bajeti kule mjengoni Idodomia.
Mbunge akiondoa shilingi kwenye bajeti ina athari gani? Na akigoma kuirudisha pamoja na marekebisho nini kitatokea?