Uchaguzi umeisha lakini kwa hapa Musoma, ni uchaguzi utakaokumbukwa sana kwa kuwa na matukio kabla na baada ya uchaguzi. Inasemekana katika jimbo hili la Musoma Mjini ni NADRA kwa mbunge kutawala vipindi viwili! Kwa mfano Ibrahim Marwa (ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Same) alikuwa mbunge kwa miaka 5 tu kabla ya kung’olewa na mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ameng’olewa na Vincent Nyerere wa CHADEMA. Sina hakika kama huyu atadumu vipindi viwili lakini wananchi wataamua hapo baadaye!!!
CHADEMA ilinyakua jimbo na udhibiti wa halmashauri ya Manispaa kwa kupata Madiwani 8, CUF 2 na CCM 3 ambapo mmojawapo wa CCM amekataa kutia saini kuwa AMESHINDA!!!!! Jamani fursa inakuja weye waikataa?….lol! NItalijadili hilo baadaye panapo majaaliwa!
Pata taswira za ushangiliaji ushindi siku ya tarehe moja mwezi Novemba kwa kuwa mbunge huyu mteule alikuwa wa kwanza kutangazwa kwa nchi nzima…usiniulize kwa nini labda ntakueleza tutakapoonana kwenye kahawa….lol!
Mamia ya washabiki wakielekea nyumbani kwa mbunge Mteule kujiunga na wenzao kushangilia.
Mashabiki wakishangilia na kuufanya mji wa Musoma kuzizima kwa muda
Palikuwa hapatoshi!
Nadhani kwa mara ya kwanza (kwani sijawahi kuona ama kusikia live) staili mpya ya ushangiliaji ikaonekana hapa mjini! Nyuma ya gari na picha inayofuata wakaonekana mashabiki wakiwa na jeneza la kiislam lilotengenezwa kwa neti ya kuzuia mbu na likiwa na picha ya mgombea wa CCM!!!! Hawakuishia hapo pikipiki moja almaarufu ‘bodaboda’ ilionekana ikiwa imebeba jeneza litumikalo na wakristo huku wakiimba kuwa wanakwenda kumzika mgombea aloshindwa!
Binafsi sikufurahia jambo hilo lakini ni historia ya kukumbukwa mwaka huu!!!!