Baba Askofu Michael Msonganzila wa jimbo Katoliki la Musoma akiendesha misa ya kumbukizi la miaka 11 ya kifo cha Mwl. J.K. Nyerere iliyofanyika jana huko Butiama. Katika homilia yake Askofu Msonganzila alizungumzia wasifu wa Baba wa Taifa mintaarafu uchaguzi ujao. Mambo kama ustawi wa watu, amani, heshima na haki kwa wote vilitawala maisha ya Mwalimu. Mambo muhimu aliyosema:
“pengo kati ya walionacho na wasiokuwa nacho linaongezeka. Kadiri linavyoongezeka ndivyo na wasiokuwa nacho wanavyo jawa na hasira kwa kuwa wanafalsafa wanasema kuwa mtu mwenye njaa huwa na hasira na siku zote hasira itajitokeza nje kwa namna mbalimbali”
“Mwalimu aliwaweka watu kama hatma ya kila jambo alilokuwa analifanya ktk nchi hii maendeleo ya watu) tofauti na viongozi wa sasa wanawatumia watu kama nyenzo/vyombo vya kutekeleza matakwa/tamaa zao mbaya kisiasa”
“rushwa na maovu mengine yanatamalaki katika jamii yetu kwa kuwa kuna tamaa mbaya za aina mbalimbali. Kwa bahati mbaya viongozi wa dini wakiyazungumzia wanaambiwa wavue majoho waingie kwenye siasa. mbona tukifanya kazi za jamii kama kujenga hospitali na mashule tunasifiwa, kwa nini katika hili la kukemea maovu tuambiwe tukavue majoho tufanye siasa”
“mchakato wa kumtangaza Mwalimu kuwa Mtakatifu uachwe utendeke kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kanisa katoliki na usiingiliwe kwa namna yoyote ile ili uamuzi utakapotolewa uwe ule ambao unathibitishwa bila shaka yoyote”
Umati wa watu ukiwa kaburini mara baada ya misa kwa sala na maombi.
Watu wakijumuika Mwitongo.
Kundi la baadhi ya wana maombi kutoka Dar Es Salaam wakiongozwa na Pd Felician Nkwera na Sr. Dina nao walikuwa miongoni mwa wageni waliofika kwa ajili ya kuungana na Mama Maria Nyerere na familia yake ktk mkesha na misa ya kumbukumbu hiyo.