
Pamoja na salamu za Mei Mosi hapo kesho, nawatakia wikiendi njema na kibonzo hiki!
Tuanze safari yetu ya pamoja kutafakari hali na mustakabali wa maisha ya Kijijini Kwetu. Haina maana ya kule nitokako bali hata kwako pia. Yawezekana huna ukakika kama sitafika! Karibu sana

mbele yake.
Jana nilihudhuria maziko ya Mama Mkwe wa mdogo wangu alofariki kwa tatizo la INI akiwa na miaka 84 huko kijijini kwetu.
Nina shida na makampuni yanayouza mbegu. Makampuni hayo kama Mosanto nk yote toka nchi za mabwanyenye wa dunia hii. Sasa tumefikia hatua ambapo mbegu hizi zinakuwa zimebadilishwa vinasaba (genetically modified).
Wadau mbalimbali duniani wanapinga hoja ya watu kupewa bure ama hata kwa kununua kwa kuwa si endelevu.Hizi ni mbegu unazoweza kuzipanda kwa msimu mmoja tu na wanafanya hivi ili kutukamua hata vile vipesa viduchu tunavomenyeka kuvitafuta.
Mbali na hayo wafanyabiashara hawa hawajali kabisa mambo muhimu ya kuzingatia.
1. Hawajali juu ya mbegu zenye kuhimili mabadiliko ya hali ya tabia-nchi (climatic Change) na ukame
2. Hawajali kabisa ladha ya hicho kinachozalishwa. Mtakubaliana nami kuwa zamani mahindi yetu yalikuwa na ladha tamu tofauti na ladha ya mahindi haya tulionayo siku hizi. Nakumbuka enzi zile miaka ya 70 ukipita nyumba ya jirani walipopika ugali wa mahindi utajua tu kutokana na harufu na pia tulikuwa tunakula ugali bila hata mboga kutokana na utamu/ladha yake tamu. Wenyewe tuliita 'reghureghu'.
3. Hawajali kabisa uendelevu wa mtu maskini na pia uwezo wa wananchi wetu wa kuchagua na kutumia mbegu zetu wenyewe. Wanasisitiza kuwa zetu hazifai. Zamani (na jamii chache sasa zimebaki na utaalamu huu) tulikuwa tukishavuna tunachagua mbegu na kuziingika juu ya paa juu ya meko ili kuzuia wadudu wanaobungua mbegu hizo. Na msimu ukifika anachukua mbegu hapo alipoziweka na kuzipeleka shambani. Kwa wale wasiokuwa na mbegu bora iliruhusiwa kwa jamii kubadilishana mbegu kulingana na mahitaji.
Sasa hali si hivo...sasa tunatakiwa kununua kila mwaka kwa kuwa hizi za madukani huwezi kulima misimu miwili mfululizo.
4. Hawaangalii aina ya udongo tulio nao. Na matokeo yake ni kwamba kwa kuwa zinatumia madawa/mbolea za viwandani kwa kiwango kikubwa.
Hapa ndo kuna changamoto kubwa kwa KILIMO KWANZA.
Kwamba kila mwaka mtu wa kijijini auze mbuzi wake ili anunue mbegu na pia mbolea.
Huu ni UTUMWA MPYA!

Ndiyo! Ni vigumu kuwa elewa wanasiasa!
Kitambaa cha 'Tambiko'
Watu wote walopita eneo hilo walionekana kushangaa na kupigwa na taharuki na hakuna aliyethubutu kuzichukua pesa hizo! Hata niliposhuka katika 'bodaboda' langu ili kuchukua picha hizi kwa kutumia simu yangu watu walinishangaa wakiwa na sura za wasiwasi!
Barabara zetu zina ubora unaotakiwa? Bidhaa hazina ubora, vipi kuhusu watengenezaji?