Friday, March 19, 2010

Enzi zile za Kutokuwa na Housegirl!

Nilifukiwa nusu mwili ili kuwawezesha wazazi kulima

kwa raha bila karaha!





Nakumbuka simulizi za baba na mama yangu wa kule Ryakahenge enzi hizo nimezaliwa hakukuwa na 'Housegirls’! Wananisimulia kuwa wakati wakiwa wanakwenda shambani ilikuwa inawapasa kuchimba shimo na kunizika nusu kama njemba hapo juu kwenye picha.


Hapo ningelia weeeee mpaka basi. Ningejinyamazia na kula mchanga kama sina akili njema. Thanks God enzi hizo LABDA magonjwa hayakuwapo kwa kuwa tulikuwa hata twatembea uchi bila nguo na hakuna cha NYUMONIA wala nini. Siku hizi mtoto atembee kifua wazi tu utasikilizia muziki wake…lol! Sijui ndo utawazi huo ama?



Sasa enzi hizi katika malezi ya watoto kuna kitu kinatisha sana. Wengi wetu tumeajiri wasichana wa kazi watusaidie kulea wakati tumejielekeza katika kazi za kujitafutia riziki.

Matokeo yake tumesikia madhara kibao yatokanayo na malezi kwa watoto ama hata vifo kwa watoto kwa sababu ya kutopata matunzo muhimu kama chakula, usafi na kadhalika.

Tumesikia pia kuwa wasaidizi hawa wa ndani aidha wakiwaleta watu (vijana wa kiume) nyumbani ama akimfungia mtoto/watoto na kutokomea kwenda misele na hivo kuhatarisha usalama wa watoto na mali.


Swali: Katika nchi nyingine baba na mama wanapata likizo ya uzazi tofauti na huku kwetu.

Je ni njia ipi bora ya kumpa matunzo mtoto mdogo kabla hajajitegemea ikitiliwa maanani kuwa baba na mama wana majukumu mengi ya kikazi?

Tuesday, March 16, 2010

Ati kuna Ukweli katika hili?



Ati wa aina hii ndo hupendwa na wanaume wanene?



Leo nimepata ujumbe wa simu toka kwa msomaji wangu mmoja wa Uru huko Moshi akiuliza kama ni kweli kwamba akina dada wembamba a.k.a ma-miss ama vipotabo huolewa na wanaume wanene zaidi wakati akina dada wanene a.k.a tipwatipwa huolewa na wanaume wembamba.

Je hii ni kweli?


Na kama ni kweli kuna sababu yoyote ile ya msingi ya kufanya hilo suala liwe hivyo?

Friday, March 5, 2010

Umesikia juu ya Wanaume Laptop?

Huyo ni mwanaume akiwa bize na laptop yake ktk hotel ya Beach Comber jirani kabisa na Whitesands Hotel- Dar leo hii hii!

Kila mwaka tarehe 14 Februari duniani kote huwa inasherehekewa sherehe ya Valentino. Pamoja na kuwa muumini wa dini ya kikristo inayoamini juu ya watakatifu kama Mt Simon, sina hakika na maana ya siku hii. Nasema hivyo kwa sababu yawezekana maana halisi ya siku hiyo ishapitwa na wakati na sasa yanafanyika ambayo hayakuwako ama hayakupaswa kuwako!

Nadhani nyote mnajua jinsi inavyosherehekewa kwa mbwembwe na maraha!

Lakini huko Shinyanga mjini hali ilikuwa tofauti kidogo na tulivyozoea. Siku hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga ilikuwa ya aina yake ama niseme ya kipekee kwa kuwa wale tu walio katika ndoa (walipaswa kwenda na vyeti vya ndoa na PETE...lol) ndiyo walioruhusiwa kujumuika na walitoka katika takribani kata 40. Sherehe hiyo iliandaliwa na mradi wa CHAMPION. Hapo watu walifundwa na makungwi...lol

Lakini mwanamke MMOJA ndiyo aliye kuwa kungwi wa uhakika ambaye amenifanya niwashirikishe hili jambo. Alikuja na hoja ya WANAUME LAPTOP! Bila shaka mmeshawahi kusikia juu ya wanaume SURUALI..lol

Mama huyu alilalamika kuwa wababa wa siku hizi wakiwa ofisini wanakuwa na LAPTOP! Wakirejea nyumbani LAPTOP. Chumbani LAPTOP! Mama anasubiri weee lakini baba na LAPTOP. Matokeo yake ni kuwa anasinzia bila kupata chakula a.k.a njaa siku nenda rudi!

NA matokeo yake ni kuwa wanapata madhara ya kisaikolojia (?) kiasi kuwa wanakosa hisia na mama hata akishika kunako sehemu ilomfanya aje pale nyumbani anasikia 'NAMBA ULIOPIGA, HAIPATIKANI KWA SASA. TAFADHALI JARIBU TENA BAADAYE'....lol

Mama amemwaga sera kuwa wanaume inawapasa waache mara moja mtindo huo kwa kuwa wana hatari ya kuumia kiafya kwa kuwa kila wakati wanabofyabofya kiasi cha kuathiri mishipa ya neva za hisia na hivo hata asiwekeze kushika kiuno cha mamaa sawa sawa!

Hili suala la LAPTOPS limekuwa na athari kubwa kwa ndoa zetu kiasi kwamba mmoja wa wanandoa anaweza kuruka UKUTA (mwajua namaanisha nini). Kwa kuwa muda mrefu baba anakuwa na LAPTOP kiasi cha kusahau kuwajibika ipasavyo. Angalia kama hilo jamaa hapo beach. Badala ya kupumzika ili kutuliza mawazo, lenyewe na LAPTOP!

Na kimbembe kinakuja pale ambapo mama anakuwa na laptop na baba naye ana laptop. Nimezungumza na mama mmoja hapa ananambia kuwa inapotokea hivyo hali ya CHAKULA katika nyumba hiyo inakuwa ni KUBAKANA kwa kuwa kila mtu hana muda na mwenzake na wanapokutana ni chapchap bila maandalizi...lol

Kwa nini lakini iwe hivyo? ama ndo athari za utandawazi wizi tuloukaribisha kwa mbwembwe? Je kuna remedy ya tatizo kama hili?

Thursday, March 4, 2010

Raha na karaha ya Mama Mkwe!


Nimesoma katika kijiwe cha Dada Yasinta kuhusu NDOA ama NDOANO na ninajuliza maswali mengi.

kwamba wakati mwingi mawifi na wamama wakwe wanaingilia ndoa za wana wao.

Ndoa zinafikia wakati zinaparaganyika. Sasa swali hapa hii NI HULKA ya akina mama wote hata weye usomaye habari hii? Je hata kwa wenzetu weupe hali iko hivi ama ni kwa weusi tu?

Je akina baba (mzazi wa kiume wa kijana) nao wana mkono ktika uMAFYA wa mama wakwe?


Na je mama aweza kumkoromea mkwe wake wa kiume kama anavoweza kumkoromea mkwe wake wa kike?